HIV Testing in Pregnancy: Part of Antenatal Blood Tests - Swahili version

Reviewed
June 2019
This resource relates to the following topics:

Upimaji wa virusi vya UKIMWI kama moja wapo ya vipimo vya damu kwa wanawake waja wazito. All pregnant women are being offered an antenatal screening test for HIV/AIDS as part of their routine care. This web-only information in Swahili explains the test. See also the English version with photographs HE1832.

Download resource

Download PDF

Details

Reviewed
June 2019
Format
Leaflet A4
Type
PDF download
HE code
HE1928
Language
Swahili

The full resource:

Upimaji wa virusi vya UKIMWI kama moja wapo ya vipimo vya damu kwa wanawake waja wazito

Upimaji wa virusi vya UKIMWI kama moja wapo ya vipimo vya damu kabla ya uzazi

Virusi vya UKIMWI (Upungufu wa Kinga Mwilini). Ikiwa havijagunduliwa na kutibiwa, virusi hivi husababisha maradhi ya UKIMWI.

Idadi ya watu walio na virusi vya UKIMWI nchini New Zealand ni ndogo lakini idadi hiyo inaongezeka kwa hivyo wanawake wote wajawazito wanapimwa virusi vya UKIMWI kama moja wapo ya huduma kabla ya wao kujifungua. Mwanamke aliye na virusi anaweza kuambukiza watu wengine au kuambukiza mtoto wake wakati wa kuwa mjamzito, wakati wa kuzaa au wakati mtoto anaponyonya.

Upimaji wa virusi vya UKIMWI utafanywa sambamba na upimaji wa kawaida wa hali ya damu kabla ya kujifungua, upimaji wa kikundi na idadi ya damu, upimaji wa magonjwa ya ini, ukambi na kaswende. Sampuli moja ya damu yaweza kutumiwa kwa vipimo hivi vyote na vipimo hivi vinatolewa bure kwa karibu wanawake wote.

Pata habari kamili ili utoe idhini ya kupimwa

Sawa na aina zote za vipimo kwa waja wazito, ni muhimu uwe na habari za kutosha zitakazo kusaidia wakati wa kuamua kupimwa.

Ikiwa una jambo lolote ambalo ungependa kujua kuhusu upimaji wa virusi vya UKIMWI, shauriana na daktari, mkunga au mtaalamu wa afya. Unaweza pia kushauriana na mpenzi wako au jamii yako.

Una haki ya kuamua kutopimwa.

Kwanini kupimwa virusi vya UKIMWI?

Karibu wanawake wote wajawazito walio na virusi vya UKIMWI hawajui kwamba wana virusi hivyo. Kwa upimaji tu ndiyo unaweza kudhibitisha virusi hivi.

Baada ya kujua kuwa ana virusi vya UKIMWI, mwanamke anaweza kupata matibabu na usaidizi mapema. Matibabu na usaidizi huu pia atapewa mpenzi wake na jamii yake ili kupunguza uwezekano wa kuambukiza mwanawe virusi vya UKIMWI.

Idadi kubwa zaidi ya wanawake wajawazito hupatikana kuwa hawana virusi vya UKIMWI.

Je, upimaji huwa sahihi?

Upimaji huwa sahihi kabisa lakini matokeo kwa wanawake wachache yanaweza kutokuwa kamili na hivyo kurudiwa. Baada ya kurudiwa, matokeo hayo huonyesha kutokuwa kwa virusi vya UKIMWI.

Nitapate matokeo ya kupimo vyangu?

Mtaalamu wa afya aliyepima damu yako atakujulisha matokeo yako.

Mwanamke anayepatikana kuwa na virusi vya UKIMWI atapewa ushauri na usaidizi na wataalamu ili alinde afya yake, ya mwanawe, ya mpenzi wake na ya jamii yake. Mwanamke mjamzito aliye na virusi vya UKIMWI atapewa matibabu zaidi na wataalamu.

Je, matibabu ni dhabiti?

Matibabu ya kuzuia mtoto kuambukizwa virusi ni dhabiti kabisa. Bila matibabu haya, kuna uwezekano wa asilimia ishirini na tano ya mtoto kuzaliwa na virusi vya UKIMWI. Matibabu haya hupunguza uwezekano wa mtoto kuzaliwa na virusi vya UKIMWI na kufikia chini ya asilimia moja (1%).

Matibabu na usaidizi wa mapema ni muhimu kwa wanawake walio na virusi vya UKIMWI ili wawe na afya njema.

Matibabu ni yapi?

Wanawake wajawazito walio na virusi vya UKIMWI watapewa matibabu na mahitaji mengine kama ifuatavyo:

  • dawa wakati wakiwa wajawazito na wakati wa kujifungua ili wawe na afya nzuri kwa muda mrefu na kuzuia wao kuambukiza watoto kabla ya kujifungua. Pia watashauriwa kuhusu njia salama za kujifungua
  • dawa za mtoto atakazo tumia kwa wiki chache baada ya kuzaliwa
  • ushuhuda wa kimataifa wa sasa waonyesha kwamba matibabu kabla na baada ya kuzaliwa hayadhuru mtoto
  • mawaidha kuhusu njia salama za kumlisha mtoto.

Je, kuna siri katika upimaji na matokeo?

Matokeo yote yatakuwa ya siri.

Mwanamke aliye na virusi vya UKIMWI atapata huduma ya kitaalamu, kwa njia ya heshima na kwa siri.

Matokeo yake yatawekwa katika vyeti vyake vya utibabu na yataweza kuonwa na wanaomtibu pekee yake.

Ili kuhakikisha kwamba mradi huu ni salama na dhabiti kwa wanawake, uchunguzi utafanyika katika ngazi ya kitaifa. Matokeo ya kila kipimo yatahifadhiwa na kuchunguzwa. Wanawake walio kwenye mradi huu hawatatangazwa.

Mradi huu wa kupima virusi vya UKIMWI kwa wanawake wajawazito unaongozwa na kitengo cha upimaji katika Wizara ya afya. Lengo la mradi huu ni kugundua virusi vya UKIMWI kwa wanawake waja- wazito na kusaidia kupunguza idadi ya watoto wanaozaliwa na virusi vya UKIMWI.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mradi huu, Taifa kitengo cha Upimaji www.nsu.govt.nz

Kwa maelezo zaidi kuhusu upimaji wa virusi vya UKIMWI kabla ya kujifungua:

  • shauriana na daktari wako, mkunga au mtaalamu wa afya
  • tazama tovuti ya mradi wa Kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI – New Zealand. www.nzaf.org.nz
  • tazama tovuti ya mradi wa wanawake wenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI – New Zealand Positive Women Inc. www.positivewomen.org.nz